Zaidi ya miradi 500 imezinduliwa na serikali eneo la Pwani

Serikali ya kitaifa imezundua zaidi ya miradi 500 katika ukanda wa pwani kwa kipindi cha miaka 7 iliyopita huku baadhi ya miradi hiyo ikiwa imekamilika.

Kwenye mahojiano ya kipekee na pwanifm mratibu wa  pwani John Elungata amesema serikali imewekeza miradi ya mabilioni ya pesa kwa lengo la kuimarisha uchumi wa ukanda wa pwani.

Elungata amepongeza ushirikiano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi hatua ambayo ameitaja kuchangia kupungua kwa maambukizi ya virusi vya korona miongoni mwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *