Zaidi Ya Kesi Elfu Tano Za Dhulma Za Kijinsia Zimeripotiwa Yasema FIDA

Jumla ya visa elfu tano vya dhulma za kijinsia vimeweza kuripotiwa katika afisi za shirikisho la mawakili wanawake humu nchini (FIDA) kufikia mwezi Novemba pekee.

Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi mfumo wa kuskizwa kwa kesi kupitia njia ya kidijitali katika afisi za FIDA Mombasa mkurugenzi mkuu wa shirikisho hilo Anne Ireri amesema vingi ya visa hivyo vimeripotiwa hususani wakati huu wa msambao wa virusi vya korona huku akiwasihi wakenya kutonyamazia dhulma hizo zinapotokea.

Wakati huo huo Ireri amegadhabishwa na matamshi ya matusi ambayo wanasiasa wanatupiana katika majukwaa, matamshi mengine ambayo ameyataja kuwadhalilisha wanasiasa wa jinsia ya kike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *