Zahanati Kufunguliwa Lamu

Mratibu wa serikali ya kitaifa kanda ya Pwani John Elungata ameitaka serikali ya kaunti ya Lamu kuzifungua zahanati zote zilizofungwa kutokana na ukosefu wa usalama ili kurahisishia wananchi kutembea mwendo mrefu kutafuta matibabu.

Akizungumza na pwani Fm Elungata amesema njia pekee ya kuzuia msambao wa virusi vya korona ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na makao yao.

Wakati huo uo Elungata amezitaka kamati zilizobuniwa za kuwaajiri vijana kwa mradi wa kazi mtaani kuzingatia vigezo vilivyowekwa na kuhakikisha vijana wasiokuwa na namna na walio na majukumu wanafaidika na mradi huo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *