WHO Kuzuru China

Jopo la wataalamu wa shirika la afya duniani WHO linalochunguza chimbuko la ugonjwa hatari wa covid-19 litawasili nchini Uchuna Alhamisi wiki hii.

Kulingana na maafisa wa afya wa taifa hilo, wataalamu hao walitarajiwa nchini humo mapema mwezi Januari lakini kiongozi wa shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alichelewesha kuondoka kwao akihoji Beijing haikuwa imetoa idhini rasmi kwa maafisa hao kuingia nchini humo. Tume ya kitaifa ya afya iliyotangaza siku hiyo ya kuwasili kwa wataalamu hao haikutoa taarifa zaidi.

Tandavu ya Korona ilianzia kwenye mji mkuu wa eneo la kati nchini china wa Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019 kisa cha kwanza kikiripotiwa katika soko la nyama lililofungwa la Huanan.

Huku wakipania kupiga jeki utafiti amabao umekuwa ukiendelea kwa mwaka mmoja uliopita sasa, jopokazi hilo la watu 10 linatarajiwa  kutaathmini maambukizi na msambao wa ugonjwa wa covid-19 miongoni mwa wanadamu na Wanyama kwenye shughuli itakayoendeshwa kwa pamoja baina ya shirika la WHO na serikali ya Uchina.   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *