WFP Yanyukuwa Tulo la Nobeli

Tuzo la amani la Nobeli la mwaka huu imekabidhiwa shirika la chakula  la Umoja wa mataifa-WFP, kutokana na juhudi zake za kukabiliana na baa la njaa. Kamati inayoongoza utoaji wa tuzo hizo nchini Norway imesema shirika  hilo lilikuwa msitari wa mbele kuzuia utumizi wa suala la kiangazi kuwa silaha ya vita na machafuko. Tuzo hilo ni la thamani ya ‘Krona milioni-10 za Norway.’ Shirika la WFP ni mshindi wa kumi wa tuzo hilo  na limetoa shukrani za dhati  kwa kutunukiwa . Mkuu wa shirika hilo, Beasley, aliwaambia wana-habari kuwa hii ni mara ya kwanza katika maisha yake kukosa la kunena. Kinyang’anyiro cha tuzo hilo kilivutia watu-211 na mashirika 107, mwaka huu. Chini ya sheria za wakfu wa Nobeli, majina ya walioorodheshwa hayapaswi kuchapishwa kwa muda wa miaka-50

WFP Yatunukiwa Tuzo la Nobel lenye thamani ya Krona milioni-10 za Norway.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *