Wazee walalamikia kutofikiwa na fedha za wazee Taita Taveta

Wito umetolewa kwa serikali kuu kuunda mbinu tofauti ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotengwa kwa ajili ya wazee zinawafikia Walengwa.

Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch tawi la Taita Taveta Haji Mwakio anasema kuwa asilimia kubwa ya wazee hawafikiwi na fedha hizo bali wanaofaidika ni wasimamizi wao.

Haji amedokeza kuwa wakongwe wengi wanapitia hali ya uchochole licha ya kuwa serikali kuu imewatengea fedha.

Kwa upande wao baadhi ya wazee wakiongozwa na Elpina Mwambi wanasema kuwa wamejisajili katika mradi huo lakini bado hawajabahatika kupata fedha hizo na kutoa wito kwa serikali kufuatilia ili kuona kwamba fedha hizo zinafikia walengwa na usajili unafanyika kwa njia ya wazi bila upendeleo wala ubaguzi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *