Wazee Wa Zaidi Ya Umri Wa Miaka 70 Wanufaika Na Mradi Wa Inua Jamii

Wazee wenye miaka Zaidi ya 70 nchini wameanza kupokea malipo ya fedha za mradi wa inua jamii kote nchini huku wengi wakiisifu serikali kwa kuwakumbuka kwa kuanzisha mradi huo.

Wakiongea katika gatuzi dogo la Changamwe baadhi ya wanaofaidika na pesa za mradi huo wameitaka serikali kuongeza jitihada kuona kwamba pesa hizo zinawafikia wote wenye mahitaji wakiwemo walemavu, mayatima na wazee.

Aidha kuna baadhi ya waliokuwa wakipata pesa hizo za mradi huo lakini kwa sasa hawapati kwa kipindi cha Zaidi ya miaka miwili, hali ambayo imewaacha katika njia panda wakitaka kujua hatima yao.

Ramla Salim kutoka mtaa wa Noor ni mmoja kati ya wale ambao malipo yao yalikatishwa Zaidi ya miaka miwili sasa akitaka kujua hatima yake.

Hata hivyo mwenyekiti wa mradi huo katika gatuzi dogo la Changamwe Abdallah Keisi Mgenge amesema kuwa walengwa wengi wameachwa nyuma na mradi huo baada ya kuja kwa mfumo wa account base.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *