Wavuvi Wanyimwa Wanawake Wa Kuoa

Baadhi ya wavuvi mjini Malindi Kaunti ya Kilifi sasa wameingiwa na hofu kubwa wakidai kukosa wanawake wa kuoa kutokana na asili yao ya kazi.

Katibu kwenye kamati inayosimamia maswala ya uvuvi Kaunti ya Kilifi,BMU, Salim Ali Mohammed amesema hali hiyo sasa imechangia baadhi ya ndoa kuvunjika.

Salim amesema mbali na kipato chao kichache kuchochea swala hilo,tabia ya wao kufanya kazi nyakati za usiku kwa muda mrefu pia imekua changamoto.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na Yusuf Abdulrahman ambaye ana hofu huenda vijana wengi wavuvi wasipate majiko hivi karibuni kama dhana hiyo haitaachwa.

Yusufu anadai imekua vigumu kwake hata kuposa msichana akihofia kupigwa teke kutokana na kazi yake ya uvuvi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *