Watu Milioni Tisa Sudan Waathirika na Mafuriko

Shirika la umoja wa mataifa kuhusu chakula na kilimo limesema zaidi ya watu milioni tisa nchini Sudan wanahitaji usaidizi kutokana na mafuriko. Shirika hilo limeambia shirika la habari la BBC kuwa mamilioni ya ekari za mashamba zimeathirika. Sehemu kubwa ya Sudan imekuwa ikikumbwa na mafuriko kwa miongo kadhaa huku viwango vikubwa vya mvua vikishuhudiwa tangu mwezi Julai. Mvua imeanza kupungua na mafuriko yanapungua lakini sasa kuna hofu ya kutokea kwa matatizo makubwa ya kibinadamu. Shirika hilo limesema tani milioni moja za nafaka zimeharibika. Kuna hofu pia ya kutokea kwa magonjwa yanayosababishwa na maji chafu. Visa vya ugonjwa wa malaria vimeongezeka pakubwa. Shirika hilo limesema juhudi za utoaji misaada ya dharura zinatatizika kutokana na viwango duni vya ufadhili na mfumko wa bei za bidhaa nchini Sudan na pia uhaba mkubwa wa mafuta.

Mafuriko Yaathiri Tani Milioni Moja za Nafaka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *