Watoto hawana haki ya kumiliki mali ya wanaotalikiana yasema korti.

Mahakama moja nchini imetoa uamuzi kuwa watoto hawana haki kugawana mali za wazazi wao endapo watatalikiana.

Jaji  wa mahakama ya familia George Dulu kwenye uamuzi wake amesema licha ya mtalikiwa kuweza kupeana mali yake kwa watoto baada ya korti kugawana mali wakati wa kesi za utaliki,mtalikiwa hawezi itaka korti ijumuishe watoto katika ugavi huo.

Kulingana na jaji Dulu,watoto si kati ya mkataba wa maagano kati ya mume na mke wakati wa ndoa hivyo hawapaswi kudai mali itakayopatikana wakati wa mahusiano hayo na kwamba watoto wanaweza kwenda kortini kudai mali endapo wazazi wao watafariki.

Uamuzi wa jaji huyo umetokana na kesi ambapo mama mmoja anataka wanawe wajumuishwe katika kurithi mali baada ya kutalikiana na mumewe wa miaka 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *