Wapiga Mbizi Wautafuta Mwili Wa Mwanamume Aliyezama Lamu

Vitengo vya wapiga mbizi na wakazi wanaendelea kuutafuta mwili wa mwanamume mmoja aliyezama mwishoni mwa juma  kwa njia tatanishi kwenye ufuo wa bahari wa Shella katika Kaunti ya Lamu.

Shafi Omar mwenye umri wa 26 anadaiwa kutembea kandokando ya ufuo huo kabla yakuzama.

Inadaiwa kuwa huenda alitekwa na mawimbi makali ya bahari ambayo huvuma kwenye ufuo huo kila wakati.

Kamishna wa kaunti ya  Lamu Irungu Macharia amesema kwamba utafutaji wa mwili wa mwanamume huyo unaendelezwa kwa siku ya pili leo baada ya shughuli hiyo kuanza rasmi juzi jioni muda mfupi baada ya kuzama.

Ufuo wa Shella ni miongoni mwa fuo za bahari katika Kaunti ya Lamu ambazo huwa hatari kwa watu kufuatia mawimbi makali.

Fuo nyingine ni Mlango wa Tanu ulio kwenye eneo la Mkokoni, Mlango wa Bomani kwenye eneo la Kiunga, Manda Bruno, Mlango wa Kipungani, ufuo wa Manda na ule wa Mlango wa Ali ulio eneo la Kiwayu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *