Wanyama anamatumaini ya kufunzu Kombe la Dunia

Nahodha wa Harambee stars Victor Wanyama amesema kuwa anaamini kuwa Kenya itafuzu kwa fainali za kombe  la dunia mwaka 2022 nchini Katar.

Harambee Stars haijawahi kufuzu kushiriki katika fainali za kombe la dunia na itachuana na Mali, Rwanda na Uganda katika mechi za kufuzu kwa fainali hizo. 

 Wanyama, ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Montreal Impact  katika ligi kuu ya soka chini Marekani sasa amekubali kuwa Kenya imejumuishwa katika kundi ngumu lakini akasema kuwa ana matumaini kuwa Kenya itafuzu kwa fainali hizo. 

 Harambee Stars itachuana na Comoros mwezi November katika mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *