Wanawake Wanadaiwa Kuingiza Dawa Za Kulevya Lamu.

Kamanda mkuu wa polisi Kaunti ya Lamu Moses Muriithi amefichua kwamba wanawake wanatumiwa mno kuingiza dawa za kulevya katika Kaunti hiyo.

Kulingana na Muriithi, hali hiyo imechangiwa na kwamba Kaunti hiyo ina polisi wachache wa kike hivyo basi maeneo ya hatari ni wale wa kiume pekee na ambao hawana ruhusa ya kuwapekua wanawake kwenye vizuizi.

Akizungumza Mjini Lamu, Muriithi amesema visa vingi vya ulanguzi wa mihadarati Kaunti hiyo vimehusishwa na wanawake na ambao hutumiwa na walanguzi wakuu katika kusambaza dawa za kulevya kwa Vijana wa Kaunti hiyo.

Muriithi amesema polisi hawatasalia kimya huku hali hiyo ikikithiri na badala yake watawekeza mikakati tofauti ili kulinda jamii ya Kaunti hiyo na hasa Vijana wadogo dhidi ya makali ya dawa za kulevya.

Kaunti ya Lamu imetajwa kama iliyoathirika pakubwa na uraibu wa dawa za kulevya miongoni mwa Vijana huku Serikali ya Kaunti hiyo ikionyesha juhudi haba mno katika kulikabili swala hilo tata.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *