Wanawake Wahimizwa Kupigania Viti Vya Uongozi

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa Wanawake kutoka kaunti ya Taita Taveta kujitokeza kwa wingi kuwania nyadhfa za uchaguzi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mwakilishi wa wakike kaunti ya hio Lidya Haika amewataka  wanawake kupambana na wanaume katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 badala ya uteuzi wa vyama vya kisiasa.

Haika anasema mara kwa mara wanawake walioteuliwa na vyama vya kisiasa hawana sauti katika bunge la kitaifa sawa na mabunge ya kaunti.

Wakati uo huo Haika amepinga pendekezo la nafasi ya mwakilishi wa wanawake kupelekwa katika bunge la seneti akisema pendekezo Hilo halifai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *