Wanasiasa wahimizwa kutekeleza katiba kwa manufaa ya mwananchi

Wanaharakati wa maendeleo kaunti ya mombasa wamewahimiza viongozi wa kisiasa kutotia siasa katika utekelezaji wa katiba ili katiba imsaidie mwananchi mashinani.

Akizungumza na wanahabari mwanaharakati kutoka maeneo ya ziwa la ng’ombe eneo Bunge la Nyali Ben Oluoch amesema katiba imekosa kumnufaisha mwananchi kutokana na ufisadi miongoni mwa viongozi.

Oluoch aidha amewataka viongozi kuja pamoja na kuunga mkono ajenda za kumaliza ufisadi na kuleta fedha kwa mwananchi ikiwemo mpango wa upatanishi BBI pasi na kuleta siasa wala miegemeo ya kimirengo.

Aidha ameelezea kusikitishwa na wizi unaodhihirika katika wizara ya afya kuhusu pesa za corona.

Haya yanajiri huku Kenya ikiadhimisha miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *