Wanaotumia Mpaka Wa Kenya Na Tanzania Katika Eneo La LungaLungaNi Sharti Wapimwe Virusi Vya Korona.

Kamishna wa kwale Joseph Kanyiri ametoa tahadhari kwa wakaazi wanaoishi katika maeneo ya mpakani mwa taifa kuzingatia kanuni za kuthibiti maambukizi ya gonjwa la corona.

kamishna amesema hayo kutokana na mchipuko wa homa ya Corona inayoonekana kusambaa kwa kasi katika taifa jirani la Tanzania,

Aidha Kanyiri anasema kwamba wameeka maafisa wa usalama na wale wa afya katika maeneo ya mpakani katika eneo la lungalunga, vanga ili kuona kwamba wanaotumia mipaka hio wanafanyiwa vipimo.
Hata hivyo amewaonya wakaazi wa taifa la Tanzania na kenya dhidi ya kutumia njia za vichochoro kuwa hatua hio ni kinyume cha sheria na atakayepatikana atakabiliwa kisheria kwa kulenga kueneza Corona kimakusudi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *