Wananchi Wanaendelea Kuhamasishwa Kuhusu Sheria

Huku zoezi la kuhamasisha wananchi kuhusiana na shughuli za mahakama katika eneo la Pwani na taifa kwa jumla likiendelea mwenyekiti wa chama cha mawakili kanda ya pwani Matthew Nyabena ameelezea hatua ya zoezi hilo kupokelewa vyema na jamii.

Akizungumza na meza yetu ya habari Nyabena amesema kuwa wananchi katika mji wa Malindi, Mombasa na Voi wameonekana kuwa na azma ya kutaka kujua kwa kina kuhusiana na swala la kuundwa kwa katiba mpya.

Mwenyekiti huyo ametaja kuwepo na haja ya kuielimisha jamii ili kupata maarifa ya jinsi watakavyojitetea pale wanapokuwa mahakamani na hata kuondoa uoga na hofu iliyoko kwa wananchi kuhusiana na mawakili ama hata wale wanaofanya kazi katika mahakama hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *