Wananchi wahimizwa kuzingatia kanuni za afya

Wakazi wa gatuzi dogo la Chonyi wametakiwa kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi ya msambao wa virusi vya Corona unao shuhudiwa maeneo mbali mbali nchini.

Akiongea na waandishi wa habari naibu kamishna wa eneo hilo Samuel Karisa amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kuwa wakaazi wa eneo hilo wanaendelea na shughuli zao za kawaida bila kufuata maagizo ya wizara ya afya.

Aidha Karisa amewataka wakaazi wa eneo hilo kupata miongozo kutoka kwa viongozi wa kiserikali endapo watakuwa na mikutano ya aina yoyote ili kupata utaratibu unaofaa wa kuendesha mikutano hiyo.

Kamishna huyo amesema kuwa ni jukumu la kila mkaazi kujilinda dhidi ya virusi hivyo huku akisema kuwa endapo mtu atapatikana akikaidi amri za wizara ya afya,hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *