Wanaharakati Malindi wasema mimba za mapema ziangaziwe

Wanaharakati wa maswala ya kijamii mjini Malindi Kaunti ya Kilifi wamesema kuna haja ya swala la mimba za mapema kuangaziwa kikamilifu katika Kaunti hiyo .

Wakiongozwa na Helda Lameck wamesema kuwa huenda juhudi zao za kutoa hamasa kwa jamii zikafua dafu kwani wasichana katika jamii wameonekana kupokea mawaidha wanayo pewa na hata kuweka wazi baadhi ya changamoto wanazo kumbana nazo hasa wakati huu wanapokuwa majumbani kufuatia janga la Corona.

Helda ameongeza kuwa baadhi ya wasichana hao wameweka wazi kuwa wanapitia hali ngumu kwani hawajakuwa wakipata chakula cha kutosha kwani wengi wa wazazi wao wamesimamishwa kazi na hata kusambaratika kiuchumi.

Aidha mwanaharakati huyo ameelezea kuwa hali hiyo huenda ikabadilika iwapo itaangaziwa mara kwa mara kupitia jamii na idara husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *