Wanachama Wa KUDHEIHA Wapungua Kutokana Na Makali Ya Korona

Chama cha kutetea wafanyakazi wa hoteli kanda ya Pwani KUDHEIHA kimesema kumeshuhudiwa upungufu wa wanachama tangu janga la corona kuripotiwa.

Aidha chama hicho pia kimesema kumekuweko na upungufu wa mapato kwa asilimia kubwa baada ya wanachama wengi kuachishwa kazi baada ya kuathirika kwa sekta ya hoteli. 

Wengi wa wafanyikazi ambao wamefutwa kazi wamesema maisha yao yamekuwa magumu baada ya kupoteza ajira, wengi wakiendelea kuhangaika wasijiue ni vipi wataweza kukabiliana na hali hiyo ngumu ya maisha.

Katibu wa chama hicho kanda ya Pwani kaskazini Zablon Mweni, amesema chama hicho kimepata pigo baada ya wanachama wapatao zaidi ya elfu tano kupungua hadi takribani wanachama elfu mbili.

Maitha vile vile amefichua kuwa mapato ya chama pia yamepungua kwa zaidi ya asilimia 50.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *