Wamiliki wa maeneo ya burudani kupokonywa leseni Taita Taveta iwapo hawatafuata masharti asema Kamishna

Kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Rhoda Onyancha ametoa onyo Kali kwa wamiliki wa vilabu katika kaunti hiyo wanaokiuka sheria za kudhibiti msambao wa  ugonjwa wa covid 19 zilizotolewa na wizara ya afya nchini.

Onyancha anasema asilimia kubwa ya sehemu za kuuzia pombe kaunti hiyo zinakiuka saa zilizotengwa kwa ajili ya biashara hiyo jambo analolitaja kuwa ukiukaji wa sheria.

Aidha amewataka watumizi wote wa vileo wakiwemo viongozi wa kisiasa kuwajibikia saa ipasavyo huku akishinikiza serikali ya kaunti kuhakikisha kuwa wamiliki wa vilabu wanafuata sheria la sivyo leseni zao zifutiliwe mbali.

Kadhalika Onyancha aliwashauri viongozi kaunti hiyo kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia sheria ili kua mfano bora kwa wananchi na kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha sheria hiyo inafuatwa kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *