Waliokiuka Kanuni Za Wizara Ya Afya Kufikishwa Mahakamani Garsen

Zaidi ya watu 20 kufikishwa mahakamani leo mjini Garsen kaunti ya Tana Delta.

Watu hao zaidi ya 20 walitiwa mbaroni kwa kukiuka kanuni zilizowekwa na wizara ya afya katika kupambana na janga la covid 19.

Kulingana na kamanda wa polizi kutoka gatuzi ndogo la Tana Delta Salim Fundi amedokeza kuwa operesheni hiyo imeanza na itaendelea hadi pale wakaazi wa eneo hilo watakapokubali kufuata kanuni hizo.

Ameeleza waliokamatwa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Garsen na kituo cha Gamba huku tana huku wakitarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Garsen hii leo.

Vile vile amesema oparesheni hiyo inalenga maeneo ya burudani na mvinyo yanayoendelea kuhudumu kinyume cha sheria .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *