Walioiba Vipakatalishi Wanaswa Matuga

Maafisa wa polisi wamefanikiwa kuwanasa majambazi wa tatu pamoja na vipakatalishi tisa vilivyokua vimeibwa katika shule ya msingi ya Boyani.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Matuga Francis Nguli amesema polisi waliidhinisha msako dhidi ya genge hilo  baada ya usimamizi wa shule hiyo kuripoti  kuhusu  wizi uliotekelezwa shuleni humo .

Nguli amesema majangili hao wametiwa nguvuni kufuatia ushirikiano uliopo kati ya maafisa wa polisi na wakaazi wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *