Waliohusika Kwa Mauaji Ya Mzee Kilifi Kufikishwa Mahakamani

Washukiwa wanne wakuu wa mauwaji ya mzee wa kaya aliyeuliwa kwa madai ya kuwa mchawi wanatarajiwa kushtakiwa leo baada ya kukamatwa juzi katika Kaunti ya Kilifi.

Miongoni mwa wanne hao ni watoto watatu wa kiume wa mzee huyo aliyeuliwa akiwa na umri wa miaka themanini na miwili.

Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi kwenye eneo la Mtwapa Phydelis Emacar amesema kwamba wanne hao walikamatwa walipokuwa wameenda kuutoa mwili wa mzee Hannington Tinga kutoka hifadhi ya maiti ya Hospitali Kuu ya Kaunti ya Kilifi ili kuenda kuuzika.

Ngombo Tinga, Edson Nyale, Shadrack Tinga na mtu mmoja ambaye alikuwa jirani yao walikuwa wameenda kuutoa mwili wa marehemu bila idhini kutoka kwa mafisa wa polisi.

Inaarifiwa kwamba Tinga aliuliwa kwa kukatwakatwa siku kadha baada ya mtoto wake kuibua madai kwamba babake alikuwa mchawi.

Mwili wa marehemu unaendelea kuhifadhiwa katika Hospitali hiyo huku uchunguzi zaidi ukiendelezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *