Wakulima na hasara ya viboko Malindi

Wakulima katika Kijiji cha Moi, kilichoko mkabala na mto Sabaki kwenye Kaunti-ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi, wanakadiria hasara baada ya mazao yao kuharibiwa na Viboko. 

Wakulima hao wamesema juhudi za kupata usaidizi kutoka kwa maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori (KWS) hazijafanikiwa wakitishia kuwauaViboko hao.

Watu wengi wameuawa ama kujeruhiwa na Viboko hao huku mashamba yao yakiharibiwa na hawajawahi kufidiwa, kuongeza kwamba zaidi ya Viboko 40 wamekuwa wakirandaranda ovyo katika eneo hilo.

Kwamujibu wa Dominic Kiplagat Kenei wa kundi la kuwatunza VIboko katika eneo hilo kundi hilo linashirikiana kwa karibu na kundi la kimataifa la kuwatunza wanyama pori katika kutafuta suluhisho akipendekeza kuchimbwa kwa mitaro kando kando ya mashamba kama hatua ya kuwazuia wanyama hao kuingia katika mashamba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *