Wakenya Wahimizwa Kufanikisha Mpango Wa BBI

Wakenya wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuwasilisha sahihi zao ili kufanikisha kura ya maoni na kupitisha mpango wa maridhiano wa BBI.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuchukuliwa kwa sahihi hizo katika jumba la kimataifa la KICC jijini Nairobi rais Uhuru Kenyatta amesistiza kuwa mpango wa BBI ni kwa manufaa kwa wakenya wote akisema kuna haja ya kuimarisha katiba ya mwaka 2010.
Rais amesema mshikano wake na Raila Odinga umeifanya nchi hii kujiepusha na misukosuko.
Kwa upande wake kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesistiza umuhimu wa wakenya kujitokeza na kufanikisha shughuli hio huku akionekana kukinzana na wanaopinga mchakato huo wa BBI akisema mchakato huo ni wakuunganisha wakenye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *