Wakaazi Wa Taita Taveta Wahimizwa Kutokata Miti

Idara ya kuhifadhi misitu katika kaunti ya Taita Taveta imewarai wakaazi wa kaunti hiyo kuasi dhana potofu ya uchomaji wa misitu.

Afisa wa misitu kaunti hii Christopher Maina, amesema uchomaji wa misitu kunachingia uharibifu wa rasilimali za kiasili zilizoko kwenye misitu hiyo sawa kuharibu mazingira.

Hata hivyo maina amesihi wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta  Kupanda miti kwa wingi hususan majira haya ya mvua ili kuhakikisha kaunti hiyo haishuki chini ya asimia kumi eneo la misitu inayopendekezwa kisheria. 

Haya yanajiri huku madhara ya uharibifu wa mazingira katika kaunti ya Taita Taveta yakibainika wazi kutokana na ukataji wa miti kiholela hali iliyosababisha kukauka kwa mito mingi sawa na kudorora kwa kiwango cha mvua. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *