Wakaazi Wa Pwani Wahimizwa Kutoa Maoni Kuhusu Kubuniwa Kwa Chama Cha Pwani

Mbunge  wa  Kaloleni Paul Katana amewapa changamoto wakaazi wa Pwani kutoa maoni na mapendekezo ili kufanikisha kuunda chama cha Pwani.

Akizungumza na Pwani FM, amesema wakaazi hao hawastahili tu kuketi na kuwaangalia na kutarajiwa kuwepo kwa chama thabiti cha Pwani pasi wao kutoa mawazo yao.

Mbunge huyo wa Kaloleni amesema hakuna njia ya mkato na ni sharti eneo hili liwe na chama cha Pwani kitakachoshughulikia agenda za ardhi, ajira na elimu.

Kuna fununu kuwa chama cha KADU ASILI miongoni mwa vyama takriban tano vya Pwani kinapigiwa upato kukiweka dhabiti na kutumiwa ifikapo uchaguzi mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *