Wakaazi Wa Kilifi Wahimizwa Kuisoma BBI

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amewahimiza wakaazi wa kaunti hio kuhakikisha kuwa wanajisomea ripoti ya BBI iliyozinduliwa hivi majuzi ili waweze kuchukua uamuzi wa busara.

Akizungumza na meza yetu ya habari kwa njia ya simu gavana Kingi amewaomba wananchi kutotoa maamuzi yao kwa kuzingatia matamshi ya wanasiasa bali wanafaa kuhakikisha kuwa wanajisomea na kuielewa kwa undani bila kushawishsiwa na viongozi wa kisiasa humunchini.

Wakati huo huo gavana Kingi amewataka wakaazi wa kaunti ya Kilifi kuzingatia masharti ya kujikinga na maradhi ya korona huku akisema ametoa muongozo wa wafanyakazi wa serikali ya kaunti hio kufanyia kazi nyumbani baada ya baadhi yao kukutwa na virusi vya korona hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *