Wakaazi Taita Taveta Wahimizwa Kukomesha Ukeketaji

Idara ya watoto tawi la Taita Taveta wamewarai wakaazi wa kaunti hiyo kupuzilia mbali tamaduni potofu na zilizopitwa na wakati.

Afisa wa watoto katika kaunti ya Taita Taveta Juma Boga ametaja ukeketaji,dhuluma za kijinsia sawa na kunyima haki ya elimu mtoto msichana ni baadhi ya tamaduni zilizo na msingi na zinazogandamiza jinsia ya kike.

Juma anasema licha ya kuwa na sheria za kupinga tamaduni hizo ni jukumu la jamii kufanikisha makabiliano na tamaduni za kukandamiza mtoto wa kike.

Hata hivyo Juma ametaja Ukosefu wa ushahidi Kama mojawapo ya changizo za kulemeza vita dhidi ya maovu hayo kwani uovu huo unaotekelezwa kisiri. 

Kadhalika amesema kuwa mtoto wa kike anapaswa kupewa nafasi katika familia ya sauti na maoni yake kusikika na kuheshimiwa ili kupewa nafasi sawa katika katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *