Wahudumu Wa Magari Ya Uchukuzi Lamu Waonywa

Wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma kaunti ya Lamu ambao wanakiuka masharti ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona wameonywa vikali.

Haya ni kulingana na kamishina wa kaunti hiyo Irungu Macharia ambaye amesema watakaopatikana watapokonywa leseni zao huku akiongeza kuwa msako mkali utaanzishwa na asasi za usalama na wizara ya afya ili kuwachukulia hatua kali wahudumu hao.

Wakati huo huo amesema kuwa nilazima magari hayo yazingatie masharti ya wizara ya afya kama vile abiria kunawa mikono kabla ya kuabiri magari sambamba na kubeba idadi hitajika ya abiria kama ilivyoamuriwa na serikali ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *