Wahudumu wa bodaboda wamewaonya wanaoingilia sekta hio

Wahudumu wa boda boda kaunti ya Mombasa wamejitokeza kupinga usajili wa kielektroniki BIMS wakisema kuwa hawajahusishwa katika uzinduzi uliofanywa na waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiang’i hivi karibuni.

Msemaji wa wahudumu wa sekta hiyo kaunti ya Mombasa Francis Ngala amesema kuwa hawajaelimishwa kuhusu usajili huo huku wakiitaka serikali kuja mashinani ili kuwaelimisha wahudumu hao.

Aidha amesema kuwa sekta hiyo imeingiliwa na mabwenyenye wanojifanya viongozi ili kujifaidisha wao wenyewe.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wahudumu hao gatuzi dogo la Nyali Samuel Ogutu amesema kuwa wao kama viongozi wa mashinani hawataruhusu  usajili wowote kuendelea huku akimtaka waziri Matiang’i kukutana na viongozi wa mashinani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *