Wahudumu wa afya ya njanjani wadi marupurupu Kilifi

Baadhi ya Wahudumu wa afya wa nyanjani katika eneo la Mkondoni kaunti ya Kilifi wanalalalmika kutopewa chochote kitakacho watia moyo katika kuendeleza kazi wanazozifanya nyanjani.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao katika eneo hilo Justin Gona wamesema kuwa kazi wanazozifanya ni za kujitolea na kuwa hakuna marupurupu wanapokea ambayo yanaweza kuwasaidia katika kukimu mahitaji yao ya kimsingi jambo ambalo huwafanya baadhi yao kukwepa baadhi ya majukumu ili kutafuta njia zingine za kupata mapoto yao kama njia moja ya kujiendeleza maishani.

Hata hivyo Justine ameongeza kuwa wanakumbwa na changamoto nyingi wanapoendeleza huduma zao baada ya serikali kuu kuagiza kupunguzwa kwa idadi ya wahudumu hao na kusema kutokana na hatua hiyo sasa wanalazimika kutembea mwendo mrefu ili kuwahudumia wanajamii.

Aidha, mwenyekiti huyo ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuwatilia maanani wahudumu hao ili waweze kupata kipato kidogo na hata kuwapa vifaa vya kutumia katika kutoa huduma ya kwanza yaani 1st Aid

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *