Wahudumu Wa Afya Wanashughulikiwa Vyma Asema Waziri Kagwe

Wizara ya afya imeweka wazi kuwa  inawashughulikia vilivyo madaktari na wahudumu wa afya wakati huu wa kupigana na janga la korona  

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga humu nchini waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema kama serikali imeweka mkakati bora wa afya wakuwakinga dhidi ya kuambukizwa virusi vya korona huku akisema kuwa serikali imeweka bima nzuri ya afya kwa wafanyakazi wa umma humu nchini.

Kuhusu swala la hospitali kulemewa kwa kuwatibu wagonjwa wa korona waziri Kagwe amedokeza kuwa hospitali za humu nchini hazijalemewa nab ado kuna nafasi kwa hospitali nyingi kauli ambayo ameitoa siku chache baada ya madai kusambaa kuwa hospitali za humu nchini zimejaa na hazina nafasi.

Waizri Kagwe aidha amewapongeza wahudumu wa afya wa humu nchini kwa kuwa mstari wa mbele kukabili janga la korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *