Wagombea Wa Ubunge Msambweni Wawasilisha Stakabadhi Kwa IEBC

Mariam Shallet ambaye ni mgombea huru kwenye marudio ya uchaguzi mdogo wa Msambweni katika Kaunti ya Kwale amefika katika afisi ya Tume ya Uchaguzi iliyo kwenye eneo hilo kuwasilisha stakabadhi za kugombea kiti hicho.

Shallet ni miongoni mwa wagombea wanne huru ambao wanatarajiwa kuwasilisha karatasi hizo kwenye afisi hiyo hii leo.

Baadae leo mchana Feisal Bader ambaye anaungwa mkono na Naibu wa Rais William Ruto anatarajiwa kuwasilisha karatasi zake.

Bader atakuwa ameandamana na viongozi mbalimbali wa kundi la Tanga Tanga akiwemo aliyekuwa Seneta wa Mombasa Hassan Omar, Johnstone Muthama aliyekuwa Seneta wa Machakos na Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale.

Wengine ni mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa, Oscar Sudi wa Kapseret,  Didmus Barasa wa Kimilili, mbunge wa Langata Nixon Korir, Seneta mteule Christine Zawadi na Seneta Falhada Iman.

Kesho wagombea wa kiti hicho kwa tiketi ya ODM Omar Boga na wa Wiper Shehe Mahmoud wanatarajiwa kuwasilisha karatasi zao.

Uchaguzi huo ambao umewavutia wagombea kumi na mmoja utafanyika tarehe kumi na tano mwezi wa Disemba mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *