Wagombea 9 kumenyana kuwania ubunge Msambweni

Tume huru ya uchaguzi na mipaka hapa nchini-IEBC imewaidhinisha wagombezi-9 kuwania uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Msambweni unaotarajiwa kuandaliwa Disemba 15.

Wagombezi hao wameidhinishwa kuwania kiti hicho kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori mwezi Machi.

Walioidhinishwa na kupewa cheti na tume hiyo ya uchaguzi ni pamoja na Mansury A. Kumaka na Charles Bilali ambao watawania uchaguzi huo mdogo kama wagombezi huru.

Wengine ni pamoja na Ali Hassan Mwakulonda wa chama cha Party of Economic Democracy, Marere Wamwachai wa chama cha National Vision, Sheikh A. Mahmoud wa Wiper Khamis Mwakaonje Liganje wa United Green Movement, Omari Idd Boga wa chama cha ODM na Feisal Abdallah Bader ambaye ni mgombezi huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *