Wadau Wachache Wachukua Fedha Za Kufufua Utalii Pwani.

Shirika la kufadhili utalii linasema  ni wadau wachache wa sekta ya utalii waliojitokeza kuchukua fedha za kufufua utalii katika eneo la Pwani.

Mkurungenzi wa shirika hilo Jonah Erumoi amefichua kwamba wadau hao walikuwa wametuma maombi ya kufikia shilingi bilioni 1.5 kati ya shilingi bilioni 1.8 iliyokuwa imetengewa eneo la Pwani. Anaelezea kwamba anasikitika kwamba hadi kufikia sasa ni shilingi milioni 300 pekee zilizochukuliwa kutokana na wanaotuma maombi kukosa kuafikia masharti ya kupata hela hizo.

Akizungumza mjini Malindi kwenye mkutano na wadau hao, Erumoi anaelezea kwamba wengi waliweka sababu zisizofaa wakati wa kutuma maombi yao.

Duru zinaarifu kwamba wengi wa wadau walikosa kutoa lesini kutoka kwa mamlaka ya kudhibiti utalii na mamlaka ya ushuru hali inayoashiria kwamba huenda wamiliki wa hoteli wanaendesha biashara zao kinyume cha sheria.

Semi za fulusi 

Equity Financing- Kuuza sehemu ya biashara yako ili kupata mtaji wa kuanzisha biashara

Kidokezo  cha biashara-

kunapotokea mwanya wa biashara ni vyema kuuza sehemu ya biashara yako ili kuptata mtaji badala ya kuchukua mkopo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *