Waathiriwa Wa Ghasia Za Baada Ya Uchaguzi Wa 2007/2008 Waandikisha Taarifa

Zaidi ya waathiriwa 100 wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 wameandikisha taarifa katika makao makuu ya uchunguzi wa makosa ya jinai humu nchini.

Taarifa za waathiriwa hao zilinakiliwa na makachero wanaongozwa na mkurugenzi wa idara ya uchunguzi George Kinoti ambaye ameweka wazi kuwa ni wakati mwafaka wa waathiriwa hao kupata haki.

Jumla ya taarifa 118 zilinakiliwa ambapo 72 zilihusisha wale waliodhulumiwa  majumbani huku 44 wakiwa wale waliofukuzwa makwao.

Kinoti amesema kuwa serikali itahakikisha waathiriwa wote wa ghasia za baada ya uchaguzi huo wa mwaka 2007 wanapata mali zao.

Ameongezea kuwa kumekua na lalama za waathiriwa hao kutishiwa maisha lakini akaahidi kuwa haki itapatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *