Waakazi Wa Mombasa Wahamasishwa Jinsi Ya Kukomesha Ufisadi

Huku serikali ikipambana kuhakikisha kuwa inaangamiza ufisadi humu nchini,mashirika mbali mbali yamekuja na mbinu mbadala kuona kuwa wanaangamiza ufisadi katika sekta zote humu nchini.

Akiongea wakati wa warsha ya mafunzo kwa vijana katika ukumbi wa Mwidani wadi ya Airport,msimamizi wa shirika la Haki na Usawa Wilfred Olal amesema kuwa wao kama shirika wameamua kutumia Sanaa ili kuona kuwa ujumbe wa athari za ufisadi unamfikia mwananchi wa kawaida.

Aidha amesema kuwa masuala ya ufisadi yamekosa kuzungumziwa katika mitaa hali inayomfanya mwananchi wa kawaida kukosa ufahamu kuhusu ufisa

Hata hivyo amedokeza kuwa watahusisha viongozi katika warsha mbali mbali  kwa ushirikiano na wananchi ili kuangazia masuala hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *