Viongozi Wanaotoa Matamshi Ya Chuki Kutengwa

Wazee wa Kaya hapa Pwani wamesema kuwa viongozi wa kisiasa wenye wanakiuka maadili ya jamii katika uongozi wao huenda wakatengwa.

Katika kikao na wanahabari wazee hao wamesema baadhi ya viongozi eneo la pwani wamekua wakirushiana cheche za maneno majukwaani bila kuiheshimu jamii wanayoiongoza.

Kulingana na mshirikishi wa muungano wa wazee wa kaya Tsuma Kombe ni kuwa tayari wamepanga mikakati ili kuona kwamba viongozi hao wanaonywa dhidi ya mienendo yao katika uongozi.

Kwa upande wake mmoja wa wazee hao Erastus Kubo ameelezea hofu yake ya kupotoka kwa maadili ya vijana katika jamii kutokana na  hulka za viongozi wa sasa.

Aidha wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kushirikiana ili kuleta maendeleo badala ya kuvutana na kutusiana hadharani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *