Viongozi Wamuomboleza Mbunge Wazamani Mustafa Idd

Viongozi mbalimbali kakatika ukanda wa Pwani wanaendelea kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd ambaye amefariki dunia mapema leo.

Wa hivi punde kutuma risala za rambirambi ni mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ambaye ameomboleza kifo cha Idd aliyekua pia mwenyekiti wa Kampuni ya Usambazaji maji ya Coast Water.

Akiongea na meza yetu ya habari kwa njia ya simu Jumwa amemtaja Idd kama kiongozi aliyetetea maslahi ya wapwani na kuhakikisha kunakuwa na haki sawa katika maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya na mwenzake wa   Kinango Benjamin Tayari wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa shupavu na mpenda kutekeleza wajibu wake kama kiongozi.

Viongozi wengine ambao pia wametuma risala za rambirambi ni Mbunge wa Kaloleni Paul Katana.

Mustafa amezikwa nyumbani kwake Bomani eneo la Kikambala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *