Viongozi Kwale wasema mfumo mpya wa ugavi wa fedha kuathiri kaunti hiyo

Huenda mfumo mpya wa ugavi wa fedha za kaunti unaopendekezwa na tume ya kitaifa ya ugavi wa mapato CRA ukaathiri pakubwa mgao unaotengewa wadi za Kaunti ya Kwale.

Mwakilishi wa Wadi ya Mkongani Ndoro Mweruphe amesema kuwa wadi za kaunti hiyo zitapoteza shilingi milioni 60 endapo mfumo huo utapitishwa na bunge la seneti.

Mweruphe amesema kwamba kaunti ya Kwale itapoteza shilingi bilioni 1.2 hali ambayo huenda ikaathiri pakubwa bajeti ya wadi katika kaunti hiyo.

Aidha, mwakilishi huyo amesema kupitishwa kwa mfumo huo kutaathiri utekelezwaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya mashinani.

Amedai kuwa mfumo huo unaopendekeza fedha za kaunti kugawanywa kulingana na idadi ya watu kutapunguza mgao wa kaunti ya Kwale.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *