Viongozi kaunti ya Lamu wamsuta gavana Twaha

Kwa mara nyengine tena serikali ya kaunti ya Lamu imejipata njia panda baada ya viongozi wa kisiasa katika eneo hilo kumshambulia gavana Fahim Twaha kwa kile walichokitaja kuwa uzembe baada ya kubainika kuwa kaunti hiyo haina vyumba vya wagonjwa mautuni yaani ICU.

Viongozi hao wakiongozwa na mwakilishi wa kina mama cpt Ruweda Obo na seneta wa kaunti hiyo Anuar Loitiptip wamemtaksa gavana kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa kikamilifu.

Akijibu kauli hizo gavana Fahim Twaha amesema serikali yake iko mbioni kuhakikisha kuwa hospitali za king fahad na ile ya mpeketoni zinaboresha na kuwepwa vifaa muhimu vya matibabu.

Viongozi hao waliyasema hayo wakati wa mazishi ya askofu Zubedi Maina wa kanisa la full gospel aliyefariki kutokana na virusi vya korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *