Vijana Walalamikia Kunyimwa Zabuni Kilifi

Serikali ya kaunti ya Kilifi imetakiwa kuivunja kamati kuu inayohusika na utoaji zabuni kwa wenye makampuni kwenye kaunti hio.

Hii ni baada ya baadhi ya makundi ya vijana na akina mama katika kaunti ya Kilifi kulalamikia hatua ya serikali ya kaunti hiyo kukosa kuwapa zabuni za usambazaji wa bidhaa mbalimbali licha ya wao kuwa na kampuni zenye uwezo wa kusambaza bidhaa hizo.

Kiongozi  wa vijana katika kaunti hiyo Asili Randani, anasema baadhi ya vijana hawajakuwa wakipata kandarasi hizo licha ya wao kuwa na kampuni zenye uwezo kwa kile walichokisema kuwa wanadaiwa kuitishwa asilimia kumi kabla ya kupewa zabuni hizo.

Kwa upande wake Fidese Chindi naibu wa mwenyekiti wa maendeleo ya akina mama katika kaunti hiyo alisema wamekuwa wakipitia hali ngumu katika kupata kandarasi hizo kwa sababu wengi wao hawana uwezo wakulipa asilimia kumi kama.

Niswala lilomgadhabisha seneta wa kaunti hio Stewart Madzayo na kumtaka gavana wa Kilifi Amason Kingi kuivunjilia mbali kamati hio akisema kama vijana hawatapewa nafasi basi hakuna haja ya kamati hio kuendelea kutekeleza majukumu yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *