Utalii wa kuhifadhi wanyama pori wadorora Kilifi

Vituo vya kitalii vya uhifadhi wa wanyama pori kaunti ya Kilifi vimelazimika kusitisha ununuzi wa wanyama hao kutoka kwa jamii kutokana na kudorora kwa sekta ya utalii.

Msimamizi wa kituo cha Kiltalii cha Mnarani William Tsaka amesema tangu janga la kurona kuanza wamelazimika kuacha kununua nyoka na kobe kutokana na kushindwa kukidhi mahitaji yao.

Amesema kufuatia sheria za wanyama pori sasa wamelazimika kuwapunguza wanyama hao kutoka hamsini hadi 15 ili kuepuka gharama ya kuwalisha.

Msimamizi huyo ameeleza kuwa hatua hiyo imeathiri zaidi wakulima ambao walikuwa wakitegemea kuuza bidhaa zao kwa kituo hicho ili kujipatia kipato.

Anthony Gitonga ni mmoja wa wafanyibiashara hao ambaye amekuwa akinusuru nyoka kutoka kwa maboma ya watu,shule,makanisa na misikiti na kuwauza katika kituo hicho.

Gitonga anasema kwa sasa amelazimika kujitosa katika shughuli za uvuvi ili kupata kipato cha kujikimu kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *