Uingereza Kutoa Chanjo Kwa Mataifa Maskini Afrika.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepanga kutoa idadi kubwa ya chanjo ya ziada nchini humo kwenda kwa nchi maskini.

Katika hotuba kwenye mkutano wa mataifa 7 tajiri zaidi duniani – G7 uliofanyika kwa njia ya video, anatarajiwa pia kuzihimiza nchi tajiri pia kuunga mkono lengo la kutenga siku 100 mpya za maendeleo ya chanjo mpya kwa ajili ya magonjwa yanayoweza kuibuka siku za usoni.

Uingereza imeagiza zaidi ya dozi milioni 400 za chanjo mbalimbali, kwa hivyo nyingi huenda zikasalia pindi ambapo kundi la watu wazima litakapokua limefikiwa lote.

Lakini wanaharakati wa kupambana na umasikini wanasema Uingereza haifanyi vya kutosha katika kukabiliana na magonjwa kama corona.

Maamuzi juu ya ni lini na kiasi gani cha chanjo za ziada kitasambazwa kitafanywa baadaye mwaka huu.

Hilo litategemea kasi ya usambazaji wa chanjo hiyo na iwapo kutakua na hitaji la nyongeza ya chanjo hasa katika msimu wa vuli.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *