Uhaba wa fedha wakumba shule za umma

Shule zinakodolea macho changamoto za kifedha, huku wakuu wa shule wakijikuna vichwa kutokana na ukosefu wa fedha kuendesha shughuli za shule, kabla ya mitihani ya KCPE na KCSE kuanza.

Wizara ya Elimu, mwezi Januari, ilitoa nusu ya pesa za kugharamia elimu shilingi bilioni 14.6  kufadhili shule za sekondari na bilioni 4.6 kwa shule za msingi.

atibu wa kudumu wa Elimu ya Msingi na ambaye sasa amehamishwa Belio Kipsang alikuwa amesema nusu iliyobaki ingetumwa shuleni muhula huu.
Hata hivyo, ikiwa imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa mitihani ya kitaifa, wasimamizi wa shule wameanza kuelezea wasiwasi kutokana na kimya cha serikali kuhusu hatima ya mgao uliobaki.

Utoaji wa pesa kwa shule hufanywa kwa mgao wa 50:30:20 au kwa mihula kuanzia mihula.

Hii inamaanisha nusu ya pesa inafaa kutumwa katika muhula wa kwanza, asilimia 30 katika kipindi cha pili na salio la asilimia 20 katika kipindi cha tatu.

Kila mwanafunzi wa shule ya msingi hupokea jumla ya Shilingi 1,420 kwa mwaka huku wale wa shule za sekondari za bure wakipewa Shilingi 22,244.

Indimuli Kahi, mwenyekiti wa Chama cha Walimu wakuu wa Shule za Sekondari nchini Kenya, anadai kwamba fedha hizo bado hazifika katika akaunti za shule na zile zilizotolewa tayari zimeisha.

Kahi poia anasema wanafunzi wengi pia hawajaweza kulipa karo hali inayofanya shughuli katika shule nyingi kuleomazwa.

Shule za Sekondari hutegemea sana mgoa wa Serikali na karo ya moja kwa moja inayolipwa na wanafunzi kuendesha shughuli za kila siku.

Waziri wa Elimu George Magoha mwezi Januari aliwaonya wakuu wa shule dhidi ya kuwatuma wanafunzi nyumbani kwa kutolipa karo.

Kahi anaonya kwamba ikiwa hali hii haitadhibitiwa basi huenda ikaathiri wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa.

“Serikali imerudia mara kwa mara dhamira yake ya kulinda ufadhili wa shule na kuboresha hali ya maisha ya wanafunzi wasiojiweza,” Kahi alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *