Uganda Yaamua

Raia wa Uganda wanapoga kura hivi leo kumchagua Rais mpya kati ya Rais aliyehudumu kwa muda mrefu Yoweri Museveni na mwana-muziki Robert Kyagulanyi, kwa jina maarufu Bobi Wine.

Wine amejitambulisha kama mwakilishi wa kizazi cha vijana nchini humo, huku Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 76, ambaye anatafuta kuchaguliwa kwa muhula wa sita akisema anataka kuendeleza udhabiti.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi na matokeo ya uchaguyzi huo hayatarajiwi kutangazwa kabla ya Jumamosi.

Kampeini za uchaguzi huo zimeghubikwa na ghasia mbaya, ambapo watu kadhaa wameuawa.

Serikali imeagiza kuzimwa kwa mitandao yote ya kijamii, jambo ambalo Rais Museveni anasema ni kwa sababu mtandao wa Facebook uliharamisha kurasa kadhaa zilizokuwa zikiunga mkono chama chake kinachotawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *