Uchunguzi Urusi

Polisi nchini Urusi wamefuatilia safari za mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny na kile alichokunywa kabla ya kuugua katika eneo la Siberia, mwezi uliopita.

Aidha, wanajaribu kumtafuta shahidi anayesemekana kuondoka  nchini humo kwa mujibu wa wizara ya usalama wa ndani. Wizara hiyo inajiandaa kwa ombi jingine la kisheria kutoka Ujerumani ambapo Navalny alipelekwa hospitalini mwezi uliopita, baada ya kudaiwa kuwa aliwekewa sumu katika chakula.

 Kwenye taarifa, idara ya uchukuzi katika wizara ya usalama wa taifa huko Siberia, ilisema ilikuwa ikitaka kuwatuma wachunguzi kushirikiana na wachunguzi wa Ujerumani kuchunguza swala hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *