Uchaguzi Wa FKF Kuendelea

Shughuli za kuwachagua viongozi wa soka nchini katika ngazi ya kaunti zitaendelea kama zilivyoratibiwa huku kamati ya usuluhisho wa mizozo ya michezo ikisubiri kuskiza kesi ya kupinga uchaguzi huo.

Akiongea baada ya kuthibitisha uamuzi wa shirikisho la soka nchini wa kuwatawaza Gor Mahia kama mabingwa wa msimu uliopita baada ya ligi kutokamilika kutokana na msambao wa korona mwenyekiti wa kamati hio John Ohaga amesistiza kuwa uchaguzi wa shirikisho la FKF utaendelea ila huenda ukasitishwa kama maagizo ya serikali ya kukabili korona hayatafatwa kikamilifu.

Kamati hio ya usuluhisho wa michezo awali ilifutilia mbali shughuli za uchaguzi mara mbili na pia imeonya kama sheria hazitafatwa kikamilifu hakutakua na budi ila kufutilia mbali uchaguzi huo.

Uchaguzi wa kaunti umeratibiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu huku ule wa kitaifa ukifanyika tarehe 17 mwezi ujao.

Tayari majina ya wagombea wa nyadhfa za nafasi ya urai yameshachapishwa ambapo yanajumuisha aliyekua rais wa shirikisho hilo la soka Sam Nyamwea, Nicholus Musonye Herbert Mwachiro, Dan Mule, Bonface Osano, Omondi Aduda na aliyekua mweka hazina wa kitaifa wa FKF Twaha Mbarak.

Hawa wote watapamba rais wa sasa Nick Mwendwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *